Wednesday, January 10, 2007
ndugu ndabagoye kwanza nasema asante sana kwa ukaribisho wako.nimefurahi kuwa sasa mimi ni mmoja wa wanablogger hata hivyo bado mimi ni mchanga sana katika mambo haya nimebobea kwenye mambo mengine na sasa nimeona ni bora nami niingie ili niwe katika utandawizi(samahani)utandawazi.nimekuwa nikutafuta chuo kama ulichokitaja lakini hatima yake nilichofanikiwa kupata ni maajabu matupu.hapa kwa anjelika kuna elimu inayotolewa mashuleni hasa katika shule za msingi kiwango cha nane(hapa wanaita hort shule)kuna wakati mwaka jana nilijaribu kuuliza kwa mwalimu mmoja kuhusu elimu ya mahusiano akaniambia inatolewa lakini elimu hiyo niliishangaa maana si elimu ya mahusiano bali ni elimu ya kuwatahadharisha wanafunzi kuingia katika mahusiano na wageni(strangers)baada ya muda fulani nilialikwa katika kikao cha kupinga ubaguzi wa rangi dini na kabila kisha hoja hiyo hiyo akaanguka tena,cha kushangaza mjumbe mmoja alidiriki kusema ameamua kumkataza mwanae kuongea na wageni hasa watokeao Afrika,nilipata shauku ya kufahamu kulikoni na baada ya kikao nilimvamia na kuomba ufafanuzi wa msimamo wake huo.jibu lilikuwa kama ifuatavyo,nanukuu"Ich wurde mit einem afrikanischen Mann verbunden und wir hatten ein babygirl aber nachher, als er hda seine dauerhafte Wohnerlaubnis er nach links ich erreichte und andere verbindet"akiwa na maana alipata kuoana na jamaa kutoka afrika na kubahatika kupata babby girl kama anavyomwita na jamaa yule baada ya kupata kibali cha kuishi hapa akatimka na kuoa mwana mwali mwingine(alikataa kusema mke huyo mpya ana uraia wa nchi gani au ana asili ya wapi)hivyo kwake hapendi kabisa mwanae kuingia katika mkumbo wa kuoa,kuolewa,kuzaa na hatimaye kuachwa.kwazi kwako kaka
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment